Amos 9:14-15


14 aNitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa;
wataijenga tena miji iliyoachwa magofu,
nao wataishi ndani mwake.
Watapanda mizabibu na kunywa divai yake;
watalima bustani na kula matunda yake.

15 bNitaipanda Israeli katika nchi yao wenyewe,
hawatang’olewa tena
kutoka nchi ambayo nimewapa,”

asema Bwana Mwenyezi Mungu wenu.
Copyright information for SwhKC